Book Title: Tishio la Ukombozi

Subtitle: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar

Authors: Amrit Wilson and Wilson, Amrit

Book Description: Kitabu hiki kinaturudisha katika kipindi cha kusisimuwa cha miaka ya vita baridi, kipindi ambacho, sambamba na kipindi cha leo, madola ya kibeberu yamekuwa yakifanya njama za kubadilisha serikali zilizokuwepo na kuziweka madarakani zile zenye kufuata amri. Kwa kutumia kumbukumbu za picha za Johari, nyaraka za siri za Marekani na Uingereza, pamoja na mahojiano ya kina, kitabu kinatowa uchambuzi juu ya nafasi na satwa ya Chama cha Umma Party nchini Zanzibar na kiongozi wake mwenye upeo mkubwa wa mambo, Mwanamapinduzi mfuasi wa Itikadi ya Karl Marx, Abdulrahman Mohamed Babu. Kwa kuangalia kwa njia ya uwiano wa mifano inayokwenda sambamba ya wahka wa Marekani kuhusu Uchina ya Kikomunisti katika miaka ya 1960 na woga walionao hivi sasa kuhusu ushawishi wa Uchina, kitabu kinatafakari juu ya mivutano mipya iliyopo katika kupigania rasilmali za Afrika, kuundwa kwa kikosi cha AFRICOM, na jinsi Wanasiasa wa Afrika Mashariki wanavyoshiriki katika kuimarisha udhibiti wa Marekani katika nchi zao, na “Vita dhidi ya Ugaidi” katika ukanda wa Afrika Mashariki hivi sasa.

License:
All Rights Reserved

Contents

Book Information

Book Description

Amrit Wilson amechota kutoka vyanzo mbalimbali maelezo yaliyomuwezesha kuandika kuhusu Zanzibar ya nyakati za sasa. Kitabu hiki kinastahiki kusomwa na walio wengi. MAHMOOD MAMDANI, Profesa wa Masuala ya Utawala katika Chuo Kikuu cha Herbert Lehman, na Profesa wa Anthropologia katika Chuo Kikuu cha Columbia.

Amrit Wilson anafanya uchambuzi wa kina wenye kugusa hisia za msomaji kuhusu mapambano halisi na thabit dhidi ya ukoloni mamboleo kama vile ambavyo yamekuwa yakijitokeza na kuendeshwa nchini Zanzibar na Tanzania. Kwa kutumia nyaraka ambazo hapo awali zilikuwa hazipatikani, ameweza kumvuta msomaji na kumpeleka katika harakati za miaka ya 1960 ambazo zingeliweza kuleta mabadiliko ya maana ya kimapinduzi nchini Zanzibar, na yumkini pia katika sehemu nyengine za Afrika Mashariki, kama harakati hizo zisingelitekwa nyara … Baadhi ya sehemu za maelezo ya kitabu yanatowa taswira na hisia zinazomfanya msomaji kujihisi yumo kuwemo katika kusoma riwaya !

BILL FLETCHER, JR.. mwandishi na mwanaharakati, mwandishi-mwenza wa Solidarity Divided na pia mwandishi-mwenza wa Claim No Easy Victories: The Legacy of Amilcar Cabral

Kitabu hiki kinaturudisha katika kipindi cha kusisimuwa cha miaka ya vita baridi, kipindi ambacho, sambamba na kipindi cha leo, madola ya kibeberu yamekuwa yakifanya njama za kubadilisha serikali zilizokuwepo na kuziweka madarakani zile zenye kufuata amri. Kwa kutumia kumbukumbu za picha za Johari, nyaraka za siri za Marekani na Uingereza, pamoja na mahojiano ya kina, kitabu kinatowa uchambuzi juu ya nafasi na satwa ya Chama cha Umma Party nchini Zanzibar na kiongozi wake mwenye upeo mkubwa wa mambo, Mwanamapinduzi mfuasi wa Itikadi ya Karl Marx, Abdulrahman Mohamed Babu. Kwa kuangalia kwa njia ya uwiano wa mifano inayokwenda sambamba ya wahka wa Marekani kuhusu Uchina ya Kikomunisti katika miaka ya 1960 na woga walionao hivi sasa kuhusu ushawishi wa Uchina, kitabu kinatafakari juu ya mivutano mipya iliyopo katika kupigania rasilmali za Afrika, kuundwa kwa kikosi cha AFRICOM, na jinsi Wanasiasa wa Afrika Mashariki wanavyoshiriki katika kuimarisha udhibiti wa Marekani katika nchi zao, na “Vita dhidi ya Ugaidi” katika ukanda wa Afrika Mashariki hivi sasa.

AMRIT WILSON ni mwandishi na mwanaharakati. Miongoni mwa vitabu vyake ni pamoja na Dreams, Questions, Struggles: South Asian Women in Britain (Pluto Press, 2006), “Ndoto, Maswali, Mapambano: Wanawake wa Asia ya Kusini Ulaya ya Uingereza” na US Foreign Policy and Revolution: The Creation of Tanzania (Pluto Press, 1989) “Sera ya Mambo ya Nje ya Marekani na Mapinduzi: Kuundwa kwa Tanzania”

Authors

Amrit Wilson and Wilson, Amrit

License

Tishio la Ukombozi Copyright © 2016 by Amrit Wilson. All Rights Reserved.

Metadata

Title
Tishio la Ukombozi
Authors
Amrit Wilson and Wilson, Amrit
Translator
Ahmada Shafi Adam
Contributor
Tafsiri ya Kiswahili: Ahmada Shafi Adam
License

Kimechapishwa na Daraja Press

www.daraja.net

© Hakimiliki 2016 Amrit Wilson

ISBN: 978-0-9952223-2-8

Haki zote zimehifadhiwa, isipokuwa pale ilipoainishwa vyenginevyo. Hakuna sehemu yoyote ya kitabu hiki inayoweza kunakiliwa au kusambazwa kwa njia yoyote ile, ikiwa kwa mitambo au barua-pepe pamoja na fotokopi au kwa mfumo wowote wa kurekodi, kuhifadhi au kutumia maelezo, bila idhini ya maandishi ya wachapishaji.

Mfasiri: Ahmada Shafi Adam

Mchoraji-jalada: Kate McDonnell

Picha: Babu aliyotolewa kutoka gerezani Aprili 29, 1963 © Corbis

Library and Archives Canada Cataloguing in Publication

Wilson, Amrit, 1941-
[Threat of liberation.  Swahili]
Tishio la ukombozi : ubeberu na mapinduzi Zanzibar / Amrit Wilson; tafsiri ya Kiswahili: Ahmada Shafi Adam.

Translation of: The threat of liberation : imperialism and revolution in Zanzibar.
Includes bibliographical references.
ISBN 978-0-9952223-2-8 (paperback)

1. Umma Party (Zanzibar).  2. Babu, Abdul Rahman Mohamed.
3. Imperialism.  4. Revolutions–Tanzania–Zanzibar.  5. Zanzibar–
History–Revolution, 1964.  6. Zanzibar–Politics and government–1964-.
7. Zanzibar–Foreign relations.  I. Title.  II. Title: Threat of liberation.
Swahili.

DT449.Z29W55187 2016                    967.8’103                    C2016-906284-8

Publisher
Daraja Press
Publication Date
September 22, 2016
Ebook ISBN
978-0-9952223-3-5
Print ISBN
978-0-9952223-2-8